Karibu
Skrini ya kwanza mtu anapofungua app.
- 1LughaMteja anachagua Kiswahili au Kiingereza wakati wowote.
- 2Anza sasaMteja mpya anafungua akaunti kwa barua pepe au namba ya simu.
- 3Tayari nina akauntiMteja aliyesajiliwa anaingia.
Mwongozo kwa wamiliki · Oktoba 2026
Vicanox ina programu tano zinazotumia mfumo mmoja. Mwongozo huu unaonyesha kila programu kwa picha halisi kutoka kwenye toleo la majaribio. Namba za rangi ya machungwa kwenye kila picha zinalingana na maelezo yaliyo pembeni yake. Bonyeza picha yoyote ili kuikuza.
Mfumo kwa ufupi
Wateja wanatumia app ya simu au tovuti. Mafundi na wauzaji wana malango yao. Timu ya Vicanox inasimamia kila kitu kutoka lango la admin. Zote zinasoma na kuandika kwenye API moja, kwa hiyo ombi analotuma mteja kwenye simu linaonekana kwa fundi papo hapo.
Mitiririko
Kila hatua inaonekana kwa mteja na kwa fundi, na wote wanapata arifa. Kazi kubwa zinahitaji ukaguzi kwanza: fundi anatuma nukuu ya bei, na mteja anaikubali, anaomba mabadiliko au anaikataa. Mgogoro ukitokea, mteja anaripoti tatizo na timu ya Vicanox inaamua kupitia lango la admin.
Kikapu chenye bidhaa za maduka mawili kinakuwa oda mbili, moja kwa kila duka, kwa sababu kila muuzaji anasafirisha mwenyewe.
Mteja hamlipi fundi wala muuzaji moja kwa moja: analipa ndani ya Vicanox. Hii inamlinda mteja, na Vicanox inapata kamisheni yake kabla ya kuwalipa wengine.
Programu 1 kati ya 5 · Wateja
Mteja anatafuta fundi, anaweka nafasi ya huduma, ananunua vifaa, analipa, anachat na kupiga simu ya sauti au video na fundi au muuzaji. Inatumia Kiswahili na Kiingereza.
https://demo-app.vicanox.com
App ya Android na iPhone kwa wateja. Kwa sasa watu wanaijaribu kama toleo la wavuti kwenye demo-app.vicanox.com, kabla haijapanda Google Play.
Skrini ya kwanza mtu anapofungua app.
Kabla ya kutumia app, mteja anasoma kwa ufupi jinsi Vicanox inavyomhudumia na anakubali masharti mara moja.
Kuingia kwa barua pepe au namba ya simu na nenosiri.
Ukurasa mkuu baada ya kuingia.
Orodha ya mafundi wa kazi moja, waliopangwa kwa ukadiriaji.
Kila kitu kuhusu fundi kabla ya kumhifadhi.
Chini ya wasifu kuna huduma anazotoa, kila moja na bei yake.
Mteja anaeleza kazi, mahali na muda anaoupendelea. Fundi anapokea ombi na kulikubali, au kuomba kukagua kwanza na kutuma nukuu ya bei.
Kichupo cha Huduma kinaonyesha mafundi wote, waliopangwa kwa ukadiriaji.
Vifaa vya ujenzi kutoka kwa wauzaji waliothibitishwa.
Maelezo kamili ya bidhaa moja.
Bidhaa zilizochaguliwa, zimepangwa kwa kila duka.
Hatua nne: anwani, msimbo wa punguzo, njia ya kulipa na muhtasari.
Kila kitu cha mteja mahali pamoja.
Huduma zote mteja alizoweka.
Hali ya kazi na hatua anazoweza kuchukua mteja.
Vifaa vyote mteja alivyonunua.
Mteja anafuatilia oda na anathibitisha kuipokea.
Mazungumzo na mafundi na wauzaji.
Kama WhatsApp: ujumbe wa maandishi, picha, nyaraka, ujumbe wa sauti, na simu za sauti au video.
Kila jambo jipya: uhifadhi, ujumbe, oda na malipo.
Matokeo yanaonekana mteja akiandika: maneno yanayopendekezwa, kategoria, mafundi na bidhaa.
Programu 2 kati ya 5 · Wateja (kwenye kompyuta)
Mtu yeyote anaangalia mafundi na bidhaa bila kuingia. Akishaingia, anapata eneo lake la mteja lenye uhifadhi, oda, ujumbe na wasifu.
https://vicanox.com
Soko lilelile la app, kwa kompyuta na simu kupitia browser.
Kile mtu anachoona akifungua vicanox.com.
Mafundi wote, wenye vichujio pembeni.
Ukurasa wa fundi mmoja, unaoweza kushirikishwa kwa link.
Bidhaa zote za wauzaji waliothibitishwa.
Maelezo, bei, stoo, muuzaji na usafirishaji.
Mfano: kutafuta "fundi umeme" kunaleta mafundi 12.
Wateja wanaingia hapa. Mafundi na wauzaji wanapelekwa kwenye malango yao.
Baada ya kuingia: muhtasari wa uhifadhi na oda.
Maelezo ya kazi, ujumbe na fundi, na historia ya hali.
Hali ya oda, bidhaa, anwani na malipo.
Mazungumzo yote, yakiwa na kutafuta na kichujio cha ambayo hayajasomwa.
Simu, mkoa, picha, jina, nenosiri na usalama wa akaunti.
Programu 3 kati ya 5 · Mafundi
Fundi anaweka huduma na bei zake, anapokea maombi, anatuma nukuu ya bei, anapanga kazi kwenye kalenda, anajibu maoni na kuona mapato na pochi yake.
https://provider.vicanox.com
Mfano: Daniel Chacha wa Chacha Clean Homes (akaunti ya majaribio).
Muhtasari wa biashara ya fundi.
Kila ombi kutoka kwa wateja.
Maelezo ya kazi, nukuu ya bei, na historia.
Nukuu zote alizotuma, na hali zake.
Kazi zijazo kwa siku, na siku asizofanya kazi.
Huduma anazotoa, kila moja na bei.
Fundi anachagua huduma kutoka orodha ya Vicanox na kuweka bei yake.
Mapato kutoka kazi zilizokamilika.
Pesa ambayo Vicanox inadaiwa na fundi, na maombi ya malipo.
Maoni yote, yakiwa na nyota kwa kila kipengele.
Wilaya anazofanya kazi.
Hatua za kupata alama ya "Imethibitishwa".
Jinsi fundi anavyoonekana kwa wateja.
Programu 4 kati ya 5 · Maduka ya vifaa
Muuzaji anaweka bidhaa, anasimamia stoo, anapokea na kusafirisha oda, anaona wateja na ripoti za mauzo, anaweka promosheni na kuomba malipo.
https://seller.vicanox.com
Mfano: Dodoma Home Fittings (akaunti ya majaribio).
Muhtasari wa duka.
Kila bidhaa ya duka.
Bidhaa mpya inaonekana sokoni mara tu inapohifadhiwa ikiwa hai.
Kusasisha idadi kwa haraka.
Oda zote za duka.
Muuzaji anaisogeza oda hatua kwa hatua hadi ifike.
Kila aliyenunua dukani, akiwa na idadi ya oda na jumla aliyotumia.
Mapato, oda, kamisheni na bidhaa zinazouzwa zaidi.
Misimbo ya punguzo ya duka.
Jinsi duka linavyoonekana sokoni.
Programu 5 kati ya 5 · Timu ya Vicanox
Timu inathibitisha mafundi na wauzaji, inasimamia orodha ya huduma na kategoria, inafuatilia uhifadhi, oda na malipo, inatatua migogoro, inalipa mafundi na wauzaji, na inaweka mipangilio ya mfumo.
https://admin.vicanox.com
Kwa wamiliki na wafanyakazi wa Vicanox tu.
Hali ya jukwaa zima kwa mtazamo mmoja.
Kuthibitisha mafundi wapya.
Hati za uthibitisho, maelezo, kazi na akaunti.
Kuthibitisha maduka.
Kila mtu anayeweza kuingia, kwa majukumu yake.
Kila uhifadhi kwenye jukwaa.
Kila oda, ikiwa na malipo yake.
Orodha rasmi ambayo mafundi huchagua huduma zao. Ni Vicanox pekee inayoongeza huduma.
Kategoria za huduma na za bidhaa.
Kila bidhaa iliyoorodheshwa.
Maoni yote. Yaliyoripotiwa yanawekewa alama.
Uhifadhi wenye migogoro, na matatizo ya oda ambayo wateja wamepeleka kwa Vicanox.
Maombi ya malipo kutoka pochi zao.
Kuwatumia watumiaji wote, au kundi moja, ujumbe mmoja.
GMV, uhifadhi, oda na kamisheni kwa kila mwezi.
Kanuni za soko, kuingia, barua pepe na SMS, malipo, na maudhui.
Nani kwenye timu anaweza kuingia hapa.
Afya ya mfumo: nakala rudufu, barua pepe, SMS na malipo.
Kila badiliko lililofanywa na wafanyakazi: nani, lini na nini.
Majaribio
Toleo la majaribio lina data ya mfano: mafundi 117, wauzaji 18, bidhaa 128, wateja 65, maoni 830, uhifadhi 165 na oda 184. Akaunti zote za mfano zinatumia nenosiri password. Kila mtu anayejaribu apewe akaunti yake, ili mabadiliko ya mmoja yasiwaathiri wengine. Akaunti ya admin inatolewa kwa wamiliki tu, na haimo kwenye mwongozo huu.
| Aina | Jina | Barua pepe | Ingia kwenye |
|---|---|---|---|
| Mteja | Amina Salehe | amina.salehe@email.com | vicanox.com · demo-app.vicanox.com |
| Mteja | Baraka Mwita | baraka.mwita@email.com | vicanox.com · demo-app.vicanox.com |
| Mtoa huduma | Daniel Chacha (Chacha Clean Homes) | daniel.chacha@demo.vicanox.com | provider.vicanox.com |
| Mtoa huduma | John Mwakalinga (Mwakalinga Electrical) | john.mwakalinga@vicanox.com | provider.vicanox.com |
| Muuzaji | Elia Mwasomola (Dodoma Home Fittings) | elia.mwasomola@demo.vicanox.com | seller.vicanox.com |
| Muuzaji | Ramadhani Msofe (DarElectrical Hub) | info@daresupply.co.tz | seller.vicanox.com |
Hali ya sasa